Na
Bashir Yakub.
Wakati mwingine ununuzi
wa ardhi huweza
kuchukua muda. Hii ni
kutokana na mazingira ya ardhi yenyewe
inayouzwa au kununuliwa
inavyokuwa. Wakati ununuzi
unachukua muda pia
huweza kuchukua gharama.
Gharama hizi zaweza
kuwa zinatolewa na mtu
anayetaka kununua au
anayetaka kuuza.
Ifahamike mapema
kuwa ardhi hapa
tunazungumzia viwanja, nyumba
na majengo.
Swali letu litakuwa ni je gharama hizi
zinalindwaje na sheria ili
mtu asiingize gharama
halafu kuuziwa akauziwa
mtu mwingine. Kabla ya
hilo hapa chini tuzijue gharama
zinazoweza kuingizwa kabla
ya kununua.
1. GHARAMA
KABLA YA KUNUNUA ARDHI.
( i )
Mnunuzi katika kutaka
kujiridhisha kama muuzaji
kweli ni mmliki
halali na ikiwa ardhi haina
mgogoro hutakiwa kufanya
upekuzi maalum( official search). Upekuzi
huu hufanyika ardhi
na huwa ni gharama . Ada lazima
ilipwe kabla ya
upekuzi.
( ii )
Gharama za mwanasheria. Kwasababu ununuzi
ni mchakato wa
kisheria basi wanunuzi huwaingiza
wanasheria katika mchakato huu
tangu anapoiona ardhi, kuipenda na
kutangaza kuinunua kutoka
kwa mmiliki. Kwasababu mwanasheria
atampa ushauri wa
awali, atamwandalia maombi
ya upekuzi, atamsaidia
kukagua hati miliki na
mengine mengi, basi gharama za
awali kabla ya
mkataba wa ununuzi lazima hutolewa.
( iii )
Wengine huwasaidia wauzaji katika
gharama za mchakato wa kuteuliwa
kusimamia mirathi ili
waweze kuwauzia , na
wengine huwasaidia wauzaji
kuwalipia madeni ili
ardhi iwe huru
na iweze kununulika.
( iv )
Gharama nyingine huhusisha
upekuzi ( official search) BRELA
iwapo mchakato unahusisha
kampuni mbili au
hata moja. Hutakiwa
kulipia ada BRELA
ili waweze kukupatia
taarifa za uhai, ufu,
au hadhi ya
kampuni kwa muda
huo.
Gharama zote hizi
na nyingine nyingi
hutolewa na mnunuzi mtarajiwa
kwa kutegemea ahadi aliyopewa
na muuzaji kuwa
atamuuzia yeye na
si vinginevyo.
2. HATARI (RISKS) YA
KUTOA GHARAMA KABLA.
Unaweza kuwa umetoa
gharama hizi ukiamini
kabisa kuwa baada
ya kila kitu
kwenda vizuri wewe
ndiye utakayeuziwa hiyo
ardhi. Badala yake muuzaji
akapata mtu mwingine
mwenye ofa kubwa
akakukwepa na kumuuzia
huyo mtu.
Wakati huu hatajali
gharama ulizokwisha ingiza
katika mchakato wala
muda mwingi uliopoteza katika
kufuatilia mchakato. Ni
katika mazingira haya ambapo
mnunuzi hutakiwa kulindwa
na mkataba maalum
kabla hajanunua ardhi.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...