Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum Mayanga (kulia) kuwa kocha wa muda  (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
Kocha Salum Mayanga, ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars, anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa (pichani chini) ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.
Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...