Na. Lilian Lundo – MAELEZO
Mratibu Elimu Kata (MEK) ni mmoja kati ya kiungo kikubwa kati ya ofisi ya elimu ya wilaya na shule za Serikali katika ngazi ya kata ambaye ndiye mfuatiliaji mkubwa wa maendeleo ya elimu ndani ya kata.
Shughuli nyingine zinazofanywa na MEK ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya taalamu ya wanafunzi katika kata yake, kukagua ufundishaji wa walimu, kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi pamoja na kusimamia vikao mbalimbali vya shule zilizoko katika kata yake.
Asilimia kubwa ya Waratibu Elimu Kata walikuwa wanashindwa kufikia malengo ya kazi zao kutokana na changamoto ya usafiri, ambapo wengi wao walikuwa wakitumia usafiri wa baiskeli ambao ha ukuwa usafiri rafiki kutokana na kazi yao ya kukagua shule zote katika kata wanazozisimamia.
Serikali kwa kuliona hilo, kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-T) ilitoa pikipiki kwa kila MEK katika mikoa ya Dodoma, Kigoma, Lindi, Shinyanga, Simiyu na Mara ili kurahisha ufuatiliaji wa mendeleo ya shule zao kwa urahisi.
Pikipiki hizo zimeleta mafanikio kwa kupunguza idadi ya wanafunzi watoro, kiwango cha ufaulu kupanda kutokana na ukaguzi wa mara kwa mara wa walimu pamoja na matatizo kutatuliwa kwa haraka kufuatia taarifa za shule kufika ofisi za wilaya kwa wakati.
Sweetbert Malimi ni Mratibu Elimu Kata wa Sanzawa Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma anasema kwamba Pikipiki imemuwezesha kushughulikia kwa wakati matatizo yanayotokea katika shule anazozisimamia tofauti na kipindi ambacho hakuwa na pikipiki.
Anaendelea kusema kuwa, matatizo yalipokuwa yakitokea katika shule anazosimamia yalikuwa yakimsubiri MEK hata kwa mwezi mzima. Lakini sasa hivi hali imekuwa tofauti kutokana na urahisi wa kufikika kuzitembelea kutembelea shule zake hata mara mbili kwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...