Rais wa Ghana Mhe. Nana Addo Dankwa Akufo-Addo  amemtumbua Mkurugenzi wake wa mawasiliano Eugene Arhin kutokana na  udukuzi wa hotuba yake wakati wa kuapishwa na kusababisha fedheha kubwa na aibu kimataifa kwa kiongozi huyo wa nchi.
Video zikimuonesha Rais  Addo akisoma hotuba yake mara tu baada ya kula kiapo jijini Kumasi ilionesha kuwa ni ya kuiga neno kwa neno toka katika hotuba za marais wawili wa marekani, na imekuwa gumzo mitandaoni dunia nzima.
Taarifa iliyotolewa mara baada ya hayo ilisema kwamba Mkurugenzi wa Mawasilianio Bw. Eugene Arhin amefutwa kazi.
Hotuba ya Rais huyo wa Ghana imekuwa chachu ya utani kwenye tasnia ya habari duniani kote, hasa baada ya video hiyo kumuonesha Rais Addo akitamka neno kwa neno maneno ya Marais George W. Bush na Bill Clinton.
Mapema Bw. Eugene Arhin  alitoa taarifa kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Facebook akijaribu kufuta soo kwa kusema alichokosea ni kusahau kuweka chanzo cha maneno hayo.
"Nia yangu ilikuwa ni kuweka bayana vyanzo vya maneno katika hotuba ya Rais wa Jamhuri (ya Ghana) Nana Mhe Addo Dankwa Akufo-Addo, wakati wa kuapishwa kweke Jumamosi, January 7, 2017.
"Naomba radhi kewa kutotaja chanzo cha maneno hayo. Ilikuwa ni kujisahau na sio kwa makusudi. Ikumbukwe kwamba katika hotuba hiyo hiyo nilitaja vyanzo toka kwa  J.B Danquah, Dr. K.A. Busia, Dr. Kwame Nkrumah na Biblia", alisema. Lakini siko la kufa halisikii dawa. Akajikuta yeye ndiye mtu wa kwanza kutumbuliwa. 
Hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa kituko kama hicho kutokea barani Afrika. Mwaka jana baada ya kutoa hotuba yake ya kuapishwa, Rais Muhamadu Buhari alikiri baadaye kwamba sehemu ya hotuba yake ilidukuliwa toka katika hotuba ya Rais Obama wa Marekani ya mwaka 2008.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...