NAIBU waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani ametembelea Mgodi wa RZ uliofukia Watanzania 13 na raia mmoja wa Nchini China anayetambulika kwa jina la Meng Juping na kusema kuwa serikali itaendelea kuweka nguvu ili kusaidia uokoaji.

Katika ziara yake hiyo ya dharura Naibu Waziri huyo ametoa pole kwa niaba ya serikali kwa uongozi wa Mkoa, Wananchi pamoja na Mgodi huo kukumbwa na tukio hilo.

Mara baada ya kupokea taarifa ya maafa hayo, iliyosomwa na kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria, Dk. Kalemani aliutaka uongozi wa Mkoa pamoja kamati ya uokoaji kujikita zaidi kwenye shughuli ya uokojai na waachane na mambo mengine ambayo yanaweza yakasababisha zoezi hilo liwe gumu.

‘’Ndugu zangu mimi kwa niaba ya serikali kuu napenda nitoe pole kwa hiki kilichowakumba Mkoa pamoja na Mgodi lakini napenda kuwaambia kuwa Kamati ya ulinzi na Usalama pamoja natimu ya uokoaji mhakikishe mnasimamia vyema zoezi hili ili tuwaokoe ndugu zetu ambao wamo humo ndani ya shimo,’’alisema Naibu waziri Kaleman.

‘’Kingine niagize hapa hakikisheni mnatoboa shimo kwa kutumia drilling ili tupate mwanya wa kuwapatia chakula ndugu zetu ambao wamefukiwa na udongo wakati juhudi za kufukua zikiendelea ,’’aliongeza.

Akizungumza na Maduka online mapema asubuhi ya leo kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Yahaya Samamba alisema kuwa kamati ya uokozi kwa kushirikiana kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita, ilibadilisha mfumo wa uokoaji kwa kutumia wachimbaji wadogowadogo baada ya mashine za kisasa kufikia usawa mita 20 ambazo haziwezi kuhimili uzito.

‘’Mitambo hii imekomea mita 20 tumeona tutumie wachimbaji wadogo ili twende sambaba na uokoaji uliosalama..kwahiyo usiku wa jana (juzi) saa 5:00 kamili usiku tulisitisha kutumia mashie yaani Magreda kutokana na usawa tuliofikia kuwa laini,’’alisema Samamba.
Naibu waziri wa Nishati na madini Dr,Merdadi Kalemani akiwasilia katika mgodiwa wa RZ ambako kumetokea tukio la watu 14 kufukiwa na udongo wakati wakiendelea na kazi za uchimbaji.
Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lorencia Bukwimba akiwapa pole ndugu na jamaa ambao walikuja kujua kile ambacho kitaendelea kwa undugu zao.
Wananchi wakiwa nje ya Ngome ya mgodi wakifatilia kile ambacho kinaendelea
Sehemu ambayo inatumiwa kutolea udongo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Ezekiel Kyunga akiwa katika eneo la tukio akifatilia kile kinachoendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...