Mradi
umeandaliwa na AMREF shirika lisilo la kiserikali,umezinduliwa Wilayani
Handeni katika ukumbi wa Kanisa la KKT na Mkuu wa Wilaya ya Handeni
Mhe. Godwin Gondwe. Kuzinduliwa kwa mradi huo kumekuja Kufuatiwa kuwepo
kwa jamii nyingi za wafugaji na jamii nyingine za kawaida zinazodumisha
Mila potofu ya ukeketaji wa watoto na wanawake bila kutambua athari
wanazokumbana nazo walengwa. Tathmini iliyofanyika imeonesha Asilimia
70% ya wafugaji wanafanya ukeketaji na 30% ni jamii ya kawaida ambayo
inadumisha mila hizo.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo, Mhe. Gondwe alisema kuwa jamii hazikatazwi
kudumisha mila na kufanya sherehe za kimila, lakini serikali na jamii
kwa ujumla haitakuwa tayari kuona tamaduni potofu kama ya Ukeketaji
inaendelea kukumbatiwa na kuathiri watoto na wanawake wa Wilaya
Handeni.”
Aliongeza
kuwa Vitendo vya ukeketaji vinamuathiri mtoto kisaikolojia ,kiafya,
kiuchumi na Kielimu, hali inayopelekea utoro uliokithiri shuleni na
watoto wengi kutomaliza shule na kuolewa katika umri mdogo , kutokana na
mazingira wanayojengewa na mangariba wakiwa kwenye sherehe hizo za
kiutamaduni.
Mhe.
Gondwe alieleza kuwa mradi huu ambao AMREF wameuleta kwetu tuna wajibu
wa kuumiliki, kuufanya wa kwetu na endelevu hata baada ya mwaka mmoja
kufika ukomo . Alieleza kuwa Kila mtoto anahaki ya kuishi na kupata haki
zake za msingi ikiwemo elimu kama mtoto mwingine na kwamba jamii nzima
ya Handeni iungane na kutoa ushirikiano kuanzia ngazi ya vitongoji hadi
Halmashauri kwa shirika la AMREF kuondokana na vitendo hivyo kutoka 14%
iliyopo sasa hadi 0%.
Akielezea
muundo mzima wa mradi huo, Dokta Aisha Bianaku Meneja wa Mradi alisema
kuwa, Mradi huo wameamua kuuleta Handeni baada ya kufanya tahmini na
kuona kwamba katika mkoa wa Tanga ikitoka wilaya ya Kilindi, Handeni ni
wilaya inayofuata kwa kushiriki vitendo hivi vya ukeketaji. Alisema kuwa
kata tano ndizo zitakazopewa elimu na kutoa njia mbadala kwa mangariba
ambao wamechukulia kukeketa ni njia mojawapo ya wao ya kujipatia kipato.
Elimu
itatolewa kuanzia shuleni kwa waalimu na wanafunzi, mitaani , kwa
viongozi wa kata na vitongoji, matabibu wa vituo vya afya, morani na
wazee wenye ushawishi mkubwa katika jamii.
Alisema
kuwa lengo ni kuwaelimisha madhara ya vitendo vya ukeketaji na kuondoa
kabisa desturi hii ambayo inamadhara makubwa ya kiafya na kielimu kwa
ujumla kwa watoto na wanawake hasa wakati wa kujifungua. Akaongeza kuwa
AMREF imeona ni vyema kutumia jamii zetu kuleta mabadiliko katika jamii.
Mradi
huu umedhaminiwa na mdhamini anayejulikana kwa jina la Sternstunden
chini ya shirika la AMREF GERMAN ili kuongezea nguvu mradi wa kupinga
ukeketaji ambao kwa awamu ya kwanza utafanyika kwa kipindi cha mwaka
mmoja kuanzia Januari 1/2017 hadi Desemba 31/2017. Kata zitakazonufaika
na mradi huu kutokana na tathimini ya uwepo wa jamii ya wafugaji wengi
na kukithiri kwa tamaduni hii ya ukeketaji ni pamoja na Segera, Malezi,
Konje, Kwamagome na Ndolwa ambapo kiasi cha uro 176,634.22 sawa na
milioni miatatu za kitanzania zitatumika kutekeleza mradi huo.
Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akizungumza na wakuu wataalamu wa Wilaya ya Handeni wakati wa uzinduzi huo.
Kamati ya ulinzi na usalama wakimsikiliza Mhe. Mkuu wa Wilaya kwenye ufunguzi wa mradi huo.
Daktari Aisha Bianaku ambaye pia ni mratibu wa mradi akiwaelezea wataalamu kuhusu mradi na mikakati iliyowekwa kuwafikia walengwa.
Bw. Henry Bendera mwezeshaji wa mradi kutoka AMREF akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Daktari Sarafina Mkua Mratibu wa afya ya uzazi kwa mama na mtoto AMREF kitaifa akielezea baadhi ya athari za ukeketaji.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akizungumza na wakuu wataalamu wa Wilaya ya Handeni wakati wa uzinduzi huo.
Kamati ya ulinzi na usalama wakimsikiliza Mhe. Mkuu wa Wilaya kwenye ufunguzi wa mradi huo.
Daktari Aisha Bianaku ambaye pia ni mratibu wa mradi akiwaelezea wataalamu kuhusu mradi na mikakati iliyowekwa kuwafikia walengwa.
Bw. Henry Bendera mwezeshaji wa mradi kutoka AMREF akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Daktari Sarafina Mkua Mratibu wa afya ya uzazi kwa mama na mtoto AMREF kitaifa akielezea baadhi ya athari za ukeketaji.


Habari, Nilikuwa nafuatilia huu mradi wa ukeketaji. Ni mradi mzuri sana na hongereni kwa kuubuni.
ReplyDeleteHuu mradi mpaka sasa elimu yake au semina yake inatolewa kwa lugha za KIGENI hivyo kutowafikia walengwa wote. Sielewi kwanini hizi programm hazifanyiki kwa lugha ya kiswahili ambayo ndo lugha ya walengwa.Moja ya sababu hizi elimu haziwafikii walengwa ni lugha inayotumika kuwaelimisha watu kuanzia ngazi ya juu mpaka ya chini. Tubadilike ili tuweze kuwaelimisha watu wasiojua kingereza, ili tuweze kuwaelimisha wasiojua kingereza wawaelimishe wasiojua kingereza. Lets Swahili OWN this.
asanteni