Serikali imesema
imeunda Tume ya uchunguzi ya watu 12 ili kuweza kuchunguza na kubaini chanzo
cha ajali ya moto iliyotokea jana saa Tano usiku katika chumba kidogo cha
kuhifadhia mizigo kilichopo kwenye jengo la Pili la abiria (Terminal II) katika
uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Tume hiyo iliyoundwa inaongozwa na Joseph Nyahende ambae anatoka katika ofisi
za Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege nchini.
“Ninategemea kupata ripoti
ya kitaalamu kutoka kwa Tume hii, ili kutusaidia kubaini kiundani juu ya chanzo
haswa kilichopelekea moto huu”, amesema Waziri Mbarawa.
Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua sehemu ya
kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo( jana) katika Kiwanja cha
ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ,kulia ni Mkurugenzi wa Uwanja
huo Bw. Paul Rwegasha.
Mkurugenzi
wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha
akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia
leo (jana).
Mkurugenzi
wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha
akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia
leo (jana).
Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa
wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukagua chumba cha kuhifadhia abiria
kilichoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo (jana),wa kwanza kulia ni Kaimu
Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Bw. Gabriel Migire. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...