Uwanja wa Amaan, Zanzibar |
Na Humphrey Shao,
Globu ya Jamii
Ikiwa ni miezi kadhaa tangu watani wa jadi, Simba na Yanga wakutane katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom huku wakitoka suluhu ya bao 1 kwa 1 na kuacha wapenzi wa soka nchi nzima wakiwa na kiu ya kuona mmoja wa timu hiyo inamfunga mwenzake ili wataniane vizuri.
Mara baada ya mchezo huo kila shabiki alikuwa akizungumza kuwa aina mbaya tutakutana mzunguko wa pili tutakutana mzunguko wa pili na huku wengine wakisema mna bahati hakuna mtani jembe.
Ikiwa zimebakia saa kadhaa kama sio siku moja kwa timu hizi zinaptaraji kushuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar hali imekuwa kimya kwa mashabiki wa soka kusubiria mtanange huo wa aina yake.
Nathubutu kusema hii ni mechi ya kisasi ambayo ilikuwa ikisubiliwa kwa hamu na mashabiki wa soka hili iweze kuamua nani mbabe kwa miaka hii miwili ya soka . Hivyo kimeeleweka sasa ni Simba na yanga tena uwanja wa Amaan Zanzibar. Jumanne saa 2:15 usiku.
Hii ni mechi ya tano kwa watani wa jadi kwenye uwanja huo.
Mechi 2 fainali ya kombe la Kagame ambapo mwaka 1975 Yanga ilishinda 2-0, mwaka 1992 Simba ilishinda kwa penalti baada ya kutoka sare 1-1 . Simba ilishinda mechi ya ligi kuu 1-0 na fainali ya kombe la mapinduzi 2-0.
Mechi hizo nne zinaonyesha Simba ikiwa na Historia ya kuifunga Yanga mara nyingi katika Uwanaja wa Amani.
Hivyo basi tusubiri mchezo huo utakavyopigwa je Simba Historia itambeba au Yanga ndio itakuwa inafuta uteja ndani ya uwanj huu wa Amani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...