Na Is-haka Omar, Zanzibar.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wananchi, wanachama, viongozi na watumishi wa Chama na Jumuiya zake kufanya suala la Usafi wa Mazingira kuwa utamaduni wa kudumu ili kuenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa vitendo.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati akifanya usafi wa Mazingira kupitia Tawi la CCM la Afisi Kuu Zanzibar Kisiwa Ndui lililopo katika maeneo ya Ofisi hiyo, Mjini hapa.

Alifafanua kwamba suala la usafi wa mazingira nchini lifanyike kwa ushirikiano wa wananchi wote bila ya kujali tofauti zao za kidini, kisiasa na kikabila kwani panapotokea athari mbaya zinazotokana na uchafu zinawakumba jamii nzima.

Alisema usafi wa mazingira ni miongoni mwa mambo muhimu yaliyokuwa yakisisitizwa na waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, kwa lengo la kuweka mazingira katika hali ya usafi na haiba nzuri kwa kuepusha jamii na maradhi ya miripuko.

Alisema Chama Cha Mapinduzi Pamoja na kufanya kazi za kisaiasa bado kina jukumu la kuhamasisha wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kuendeleza tabia ya kufanya usafi wa mara kwa mara katika maeneo wanayoishi.

“ Nakuombeni viongozi, wanachama, na watumishi pamoja na wananchi kwa ujumla suala la usafi lianzie katika mioyo yetu hadi katika mazingira tunayoishi, ili kuweka nchi yetu katika muonekano na haiba ya kuvutia wakati wote.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai pamoja na maafisa wengine wa chama na jumuiya zake wakifanya usafi wa mazingira kwa kufyeka majani katika uwanja uliopo katika Afisi kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar.
Kaimu Mkuu wa Utawala Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, Said Omar Mwenemzi akifanya usafi katika maeneo ya Afisi hiyo.
Mwenyekiti wa Tawi la CCM Afisi Kuu Zanzibar ambaye pia ni Msaidi Katibu wa Idara ya Oganazasheni ya Afisi Kuu CCM Zanzibar, Nadra Juma Mohamed akifyeka majani katika uwanja wa ofisi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...