Taarifa
kuhusu Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na
Malawi, Tuzo za AU kwa SSRA na TRA na Mkutano wa AU-Addis Ababa
Mkutano
wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya
Tanzania na Malawi umepangwa kufanyika mjini Lilongwe, Malawi tarehe 03
hadi 05 Febuari 2017. Mkutano huo utawakutanisha viongozi na wataalamu
wa sekta mbalimbali kutoka Tanzania na Malawi.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine P. Mahiga (Mb), anategemewa kuongoza ujumbe wa Tanzania katika
mkutano huo. Aidha, Uongozi wa Mkoa wa Mbeya ambao umekuwa ukishiriki
katika vikao vya maandalizi, unategemewa kushiriki katika mkutano huo.
Lengo
la mkutano huu ni kujadili na kutathmini hatua zilizofikiwa katika
utekelezwaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Tatu wa JPCC
uliofanyika Tanzania, tarehe 24 hadi 30 Juni, 2003.
Miongoni
mwa mafanikio yaliyofikiwa kwenye utekelezaji wa makubaliano ya
mikutano iliyopita kwa upande wa Tanzania ni pamoja na; Kuanzishwa kwa
mradi wa Kituo cha Huduma za Pamoja Mipakani (One Stop Border Post –
OSBP) katika mpaka wa Kasumulu/Songwe ambao umefikia katika hatua nzuri;
Idara za Uhamiaji, Polisi na Forodha za nchi zetu mbili zinaendelea
kushirikiana katika kutoa huduma na kudhibiti abiria na mizigo katika
maeneo ya mpakani.
Pia,
Mamlaka ya Bandari Tanzania imeruhusu Mamlaka za Malawi kuwa na maeneo
yao katika bandari zetu, kwa ajili ya kuhifadhia mizigo na bidhaa
nyingine zinazopitia nchini kabla ya kwenda Malawi.
Aidha,
mkutano huo utatoa fursa kwa nchi zetu mbili kujadiliana na kukubaliana
kuhusu maeneo mapya ya ushirikiano. Miongoni mwa maeneo hayo (kwa
upande wa Tanzania) ni pamoja na: Kuanzisha ushirikiano katika sekta ya
usafiri wa majini, ambapo mbali na faida za kiuchumi, safari hizo
zitaimarisha mwingiliano wa watu na kupunguza tofauti zilizopo. Kwa hivi
sasa Serikali inajenga meli tatu, mbili kwa ajili ya kusafirisha mizigo
na moja kwa ajili ya abiria.
Maeneo
mengine ni kuanzisha Mkataba wa ushirikiano katika Sekta ya Usafiri wa
Anga (BASA); Kuanzisha mfumo wa kurahisisha ufanyaji biashara kwa ajili
ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo hasa katika maeneo ya mpakani;
Kuanzisha ushirikiano katika uhifadhi wa mazingira na masuala ya afya
ikiwemo magonjwa ya mlipuko hususan maeneo ya mipakani; na Kuanzisha
ushirikiano katika sekta ya elimu ya vyuo vikuu na vyuo vingine vya
amali.
Tangu
kuanzishwa kwa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya
Tanzania na Malawi nchi hizi mbili zimeshafanya vikao vinne vya Tume
hiyo. Kikao cha mwisho kilifanyika hapa Dar es Salaam, Tanzania tarehe
24 hadi 30 Juni, 2003 na kuhudhuriwa na viongozi na wataalam wa sekta
mbalimbali kutoka nchi zetu mbili.
Bi Mindi akimkabidhi Bi. Sarah kombe la ushindi kwa niaba ya Wizara. Bi. Kibonde aliipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Meneja wa Mradi wa Mfumo wa Forodha wa TANCIS kutoka TRA akipokea zawadi ya cheti cha ushindi kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga.
Picha ya pamoja ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje, TRA na SSRA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...