Benny Mwaipaja-WFM, Mbeya
TANZANIA na Zambia, zimetiliana saini Mikataba Minne kwa ajili ya uanzishwaji rasmi wa kituo cha pamoja katika mpaka wa Tunduma na Nakonde, kitakachoanza kufanyakazi rasmi Februari mosi mwaka huu, ili kurahisisha ufanyaji biashara kati ya nchi hizo mbili
Uamuzi wa kuanzishwa kwa huduma hiyo ijulikanayo kama One Stop Border Post, ni utekelezaji wa maagizo ya Marais wa nchi hizo Mbili, Waheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, na Edger Lungu, waliyoyatoa wakati Rais huyo wa Jamhuri ya Zambia, Edger Lungu alipofanya ziara ya kikazi hapa nchini hivi karibuni.
Mikataba iliyotiwa saini ni makubaliano ya Mwongozo wa Utendaji wa Kituo cha Pamoja cha Tunduma/Nakonde pamoja na Mfumo wa Urahisishaji Biashara kwa lengo la kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili.
Waliosaini Mikataba hiyo kwaniaba ya Serikali ya Tanzania, Mjini Vwawa, wilaya ya Momba, mkoani Songwe, ni Naibu Katibu Mkuu wa Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, huku Zambia ikiwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa nchi hiyo, Bi. Kayula Siame.
Wakizungumza baada ya kutiwa saini kwa mikataba hiyo Makatibu wakuu hao wamesema kuwa Uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja Mpakani Tunduma/Nakonde, utarahisisha ufanyaji wa biashara kati ya Tanzania na Zambia kwa kupunguza ukaguzi kwani ukaguzi utafanyika mara moja katika kituo cha kuingia badala ya kufanyika mara mbili katika nchi zote mbili pamoja na kuongeza makusanyo ya kodi
“Lengo la kituo hicho pia ni kuifanya biashara kati ya Tanzania na Zambia kuwa huru lakini ikifuata misingi na taratibu za kufanya biashara mpakani. Pia kitarahisisha biashara katika eneo la mpakani na kuvutia wananchi na wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili kutumia kituo hiki na kuepuka kutumia njia zisizo rasmi kupitisha mizigo na hivyo kupunguza ufanyaji wa biashara za magendo kama si kukomeshwa kabisa” Alisisitiza Bi. Amina Khamis Shaaban
Alisema kuwa utaratibu huo unatarajia kuona kuongezeka kwa ushirikiano kati ya taasisi za serikali za nchi hizi kwani shughuli katika kituo zitakuwa zinafanyika kwa uwazi katika eneo moja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakitia saini mmoja wa Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Tunduma/Nakonde, ifikapo Februari Mosi, 2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakionesha Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani baada ya kusainiwa ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa kituo cha mpakani cha Tunduma/Nakonde, ifikapo Februari Mosi, 2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakibadilishana Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani Tunduma/Nakonde baada ya kusainiwa ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa kituo hicho ifikapo Februari Mosi, 2017.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakitia saini moja ya mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo Cha Pamoja na Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza kufanyakazi rasmi Februari mosi, 2017.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakionesha mikataba waliyosaini ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa Kituo Cha Pamoja cha Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza rasmi Februari mosi, 2017.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakibadilishana Mikataba waliyosaini ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa Kituo Cha Pamoja na Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza rasmi Februari mosi, 2017.
Makatibu Wakuu kutoka Tanzania na Zambia wanaohusika na masuala ya fedha, biashara na viwanda wakiwa katika kikao cha kupitia nyaraka mbalimbali za mikataba ya namna ya kuendesha Kituo cha Pamoja cha Mpakani, Tunduma/Nakonde, uliofanyika Jijini Mbeya. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Miundombinu wa Zambia, Mhandisi Charles Mushota, na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais wa Zambia, Bright Nundwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...