Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Bodi ya Mahusiano ya Kigeni kwenye masuala ya Kiuchumi nchini Uturuki (DEIK) wameingia makubaliano kuanzisha Baraza la Kibiashara baina ya nchi mbili,makubaliano hayo yalifikiwa tarehe 23 Januari 2017 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye amesema Baraza hilo litakuwa na majukumu na shughuli mbalimbali kama kusaidia kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili,kutoa mchango katika kuanzisha kukuza Viwanda kupitia ushirikiano wa Teknolojia wa mashirika na Taasisi za Kiuchumi za nchini Uturuki.

Pia amesema kuratibu juhudi za pamoja kukusanya,kuunganisha,
kuniambia,kutathmini na kieneza taarifa zinazohusu biashara.Amesema Baraza hilo litasaidia kutambua changamoto za kibiashara baina ya nchi hizo mbili na kwenye ushirikiano Kiuchumi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Reginald Mengi amesema kuwa Baraza hilo la Kibiashara baina ya Uturuki na Tanzania litagawa katika kamati za Kitaifa mbili.Kila kundi litakuwa na Wanachama wake na Taasisi  za Kiuchumi au za Kibiashara.

Amesema kuwa Kamati hizo ndogo za Baraza zinatarajiwa kukutana angalau Mara moja kwa Mwaka,kutazama na kujadili mafanikio ya Baraza kwenye masuala ya Kibiashara,Uwekezaji,
Teknolojia baina ya nchi hizo mbili.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini,Reginald Mengi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Uundwaji wa Baraza la Kibiashara baina na Tanzania na Uturuki.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF,Godfrey Simbeye akizungumzia majukumu ya Baraza lilioundwa kati ya nchi mbili za Tanzania na Uturuki.Kushoto ni Mwenyekiti wa TPSF,Reginald Mengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...