Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Renatus Mpatili (mwenye tai)akiangalia vitu mbalimbali vilivyoandaliwa na wahitimu wa mafunzo ya VETA katika mahafali yaliyofanyika katika Kanisa la Christian Center Tabata jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KUKUA kwa uchumi wa nchi kunatokana na kuwa watu wenye ujuzi mbalimbali na ukatumika katika kuleta maendeleo ya ukuaji wa uchumi huo.
Akizungumza katika mahafali ya Watu waliopata ujuzi kupitia mafunzo ya VETA yanayoendeshwa nchini, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Renatus Mpatili amesema kuwa ujuzi walioupata kupitia VETA ufanye kazi ya kuzalisha na kuanzisha biashara itakayoleta manufaa.
Amesema kuwa VETA ina mipango mizuri ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na ujuzi ambao utafanya watambulike katika kuendesha shughuli mbalimbali ikiwe ya kujiajiri au kuajiriwa.
Mpatili amesema kuwa nchi ya viwanda ya awamu ya tano inahitaji wajuzi mbalilmbali watakaotumikia katika viwanda hivyo VETA wanawajibu wa kuendelea kutoa ujuzi kwa makundi mbalimbali.
Nae Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam, Habib Bukko amesema VETA inafanya kazi yake katika kuwafikia wananchi kwa kutoa mafunzo mbalimbali ili wawe sehemu ya nguvu kazi ya tifa.
Bukko amesema kwa mafunzo walioyapata wahitimu hao wakatumie vyeti vyao katika kzalisha kila ambacho wamekisomea na kuweza kubadili maisha yao na taifa kwa ujumla.
Wahitimu wakiwa wameandaa vitu mblimbali katika mafunzo ya siku 10 waliopewa na VETA katika mahafali yaliyofanyika katika Kanisa la Christian Center Tabata jijini Dar es Salaam.
Mhitimu akisonga ugali wa lishe kwa mafunzo waliopata na VETA katika mahafali yaliyofanyika katika Kanisa la Christian Center Tabata jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahitimu katika mahafali katika mahafali yaliyofanyika katika Kanisa la Christian Center Tabata jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Renatus Mpatili (mwenye tai)akiangalia katika mahafali yaliyofanyika katika Kanisa la Christian Center Tabata jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...