Na Rose Msoka, Zanzibar
Wananchi wa Zanzibar leo wamejitokeza kwa wingi kwenye
sherehe za uzinduzi wa maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya
Zanzibar, yanayoendelea kwenye viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
Maonesho hayo yamezinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, ambaye pamoja na mambo
mengine amesisitiza Taasisi za Serikali na binafsi kutumia vema fursa ya
maonesho kujitangaza na kuonyesha shughuli wanazofanya kwa wananchi.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni miongoni mwa Taasisi
zinazoshiriki maonesho hayo ambapo pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu
umuhimu wa Vitambulisho, inaendesha zoezi la kusajili wananchi ambao bado
hawajasajiliwa, kugawa vitambulisho vya Taifa kwa wananchi waliokamilisha
taratibu za usajili, pamoja na kuonesha mfumo salama (tovuti) inayotumika
kusoma taarifa za mtu zilizoko kwenye mfumo kwa njia ya mtandao. Njia hiyo
itawezesha wadau mbalimbali kutumia mfumo huo kuhakiki taarifa za mwananchi
mwenye kitambulisho kabla ya kumpatia huduma.
Banda la NIDA limekuwa moja ya mabanda ya kuvutia, ambapo
wananchi wengi wamekuwa wakitembelea
shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye viwanja hivyo na kuonekana kuridhishwa
na huduma zinazotolewa na NIDA.
Maonesho ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar
yameanza tangu Jumamosi tarehe 07 Januari 2017 yakihusisha Taasisi mbalimbali
za Serikali zikiwemo Taasisi za Muungano, mashirika na Taasisi binafsi na
yanatarajiwa kumaliza Jumamosi tarehe 14/01/2017.
Wafanyakazi
wa NIDA wakiwa katika picha ya pamoja katika Banda lao la maonyesho katika viwanja vya maonyesho vya Biashara vya Maisara
Zanzibar tayari kuhudumia wananchi
watakaohudhuria.
) Ofisa
wa NIDA Ng Abdulaziz Juma Mtumwa
akimkabidhi Dada Lidia Adminic Kaguo Kitambulisho chake katika Banda la
Maonyesho wakati maonesho ya sherehe za Mapinduzi Zanzibar yakiendelea
kwenye viwanja vya Maisara
Kaimu Meneja
wa kitengo cha Operesheni Zanzibar Ndg. Abdallah O. Mmanga akitoa elimu
juu ya matumizi ya Vitambulisho Vya Taifa kwa wananchi waliojitokeza katika
viwanja vya Maonyesho vya Maisara Zanzibar
Bi.
Shau Mwalim Haji akimsajili mwananchi
aliejitokeza katika maonyesho ya Biashara ya Maisara.
Wananchi
wakijisajili kwenye kitabu cha wageni walipofika kutembelea banda la Maonesho
la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) viwanja vya Maisara Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...