MAMLAKA ya Usimamizi wa vyombo vya usafiri wa nchi kavu na Majini (Sumatra) mkoani Tanga kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani wameanza operesheni maalumu kwa madereva wanaozidisha abiria na nauli kwenye mabasi yanayotoka  mikoa mbalimbali ikiwemo kanda ya kaskazini.

Hatua inafuatia idadi kubwa ya abiria ambao wanatoka mikoa hiyo kurejea mkoani Tanga na maeneo mengine hivyo baadhi ya mabasi wanapandisha nauli kiholea na kuzidisha abiria.

Hayo yalisemwa na Ofisa Sumatra Mkoani Tanga, Dkt Walukani
Luhamba (Pichani Juu) wakati akizungumza na mtandao huo ambapo alisema waliamua operesheni hiyo ili kuweza kudhibiti masuala hayo ambayo yamekuwa yakiwapa wakati mgumu wananchi wanaotumia vyombo hivyo kwa ajili ya matumizi yao.

Operesheni hiyo inafanyika kwenye maeneo ya Mombo,Korogwe, Mkata na Segera ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo ili kuweza kuikomesha kwa madereva wenye tabia kama hiyo.

Dkt Walukani alisema katika kuhakikisha wanazibiti operesheni hiyo hivi sasa wanamshikilia dereva wa basi la Hood Issa Kayela (30) linalofanya safari zake kutoka mkoani Arusha kuelekea Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga kwa kosa la kuzidisha abiria zaidi ya idadi aliyotakiwa kubeba.

Alilitaja basi hilo lilikuwa na namba za usajili T.779 AVL Scania aina ya Torino lilikuwa likitokea mkoani Arusha kuelekea Mbeya ambapo baada ya kumkamata walimpelekwa mahakamani na baada ya kufika huko akukosa dhamana amerudishwa mahabusu na baade ya wiki mbili anatarajiwa kupandishwa kizimbani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...