KAMPUNI
kitalii zilizo chini ya Friedkin Conservation Fund (FCF) Tanzania
iliyowekeza katika pori la Makao wilayani Meatu na Maswa Mkoani Simiyu
imechangia mifuko 3000 ya saruji na mabati na 1000 kusaidia ujenzi wa
shule za sekondari wilayani humo. Misaada hiyo yenye thamani ya zaidi ya
sh milioni 70 imetolewa na kampuni hizo ikiwa ni kuunga mkono mkakati
wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli kuendeleza elimu
ya hasa katika maeneo ya wafugaji ambako kampuni hizo zinafanya shughuli
za uwindaji wa kitalii.
Kampuni
zilizokabidhi misaada hiyo juzi katika sherehe zilizofanyika mjini hapa
ni pamoja na Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers ambazo kwa pamoja
zimetoa saruji hiyo yenye thamani ya sh milioni 48 na mabati yakiwa na
thamani ya sh milioni 25. Vifaa hivyo vya ujenzi vitatumika kujenga
vyumba vya madarasa na mabweni kwa ajili ya shule zitakazotumiwa na
watoto wa jamii za wafugaji zinazoishi jirani na maeneo ya shughuli za
uwindaji wa kitalii wilayani Meatu katika mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) akifurahia tamko la
Mkurugenzi, Abdulkadir Mohamed (hayupo pichani) kuahidi kuongeza msaada
wa mabati 1000 huku Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack
akikabidhiwa kipaza sauti kurudia kauli ya neema za mabati 1000 toka
FCF


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...