Tangu
kuingia madarakani kwa awamu ya tano ya uongozi wa nchi yetu, msisitizo mkubwa
umewekwa katika kutekeleza ahadi ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard
gauge.
Kwa kulitambua hilo mwaka wa fedha 2015/2016 Kampuni Hodhi ya
Rasilimali za Reli (RAHCO) ilianza
maandalizi ya Ujenzi wa reli mpya ya standard gauge kwa kuanza kuandaa makabrasha ya zabuni za kuwaajiri
mkandarasi wa ujenzi wa reli ya kati pamoja na mshauri mwelekezi mnamo mwezi
Mei, 2016 na hatimae, Zabuni ilitangazwa tarehe 9 Septemba, 2016 kwa kipande
cha Dar es Salaam hadi Morogoro na tarehe ya kurudisha zabuni ilikuwa 6
Disemba, 2016.
Wakandarasi
40 walinunua zabuni na baada ya tathmini ya zabuni, Ubia (JV) kati ya YAPI
MERKEZİ İNŞAAT VE SANAYI A.Ş. (Uturuki) MOTA-ENGIL, ENGENHARIA E na
CONSTRUÇÃO ÁFRICA, S.A. (Ureno) ilionekana kukidhi vigezo vya kiufundi na
kifedha.Timu ya watalaamu ilitumwa kutembelea miradi
aliyopata kuitekeleza huko nchini Uturuki, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Msumbiji
na Afrika Kusini na kujiridhisha. Baada ya majadiliano
yaliyofanyika kati ya tarehe 21 january, 2017 mpaka 2 Februari 2017 hatimaye
maafikiano ya mkataba yalifikiwa kufanya ujenzi kama kama ifuatavyo:-
- Kilometa
205 za njia kuu na Kilomita 95 za njia za kupishania treni na maeneo ya
kupangia mabehewa jumla kilometa 300, kwa uzani wa tani 35 kwa ekseli,
- Ujenzi
wa miundimbinu ya umeme, Dar-Morogororo na kwenye njia za kupishania na
kupangia mabehewa ya treni,
- kiwango
cha mwendo kasi wa treni kuwa kilomita 160 kwa saa,
- Stesheni
6 za abiria na 6 za kupishania treni,
- Kujenga
wigo wa kilomita 102 kwa usalama wa watu na magari lakini vivuko
vitajengwa kwa matumizi ya waenda kwa miguu na magari pamoja na mifugo.
- Muda
wa mradi ni miezi 30 baada ya kuanza ujenzi,
Leo tarehe 3 Februari, 2017, ikiwa ni miaka 112 tangu
reli ya zamani iliyopo ijengwe, serikali ya awamu ya 5 imeamua kujenga reli
mpya ya standard gauge kwa mizigo tani milioni 17 kwa mwaka kwa treni ya umeme
yenye mwendokasi wa kilometa 160 kwa saa na miundombinu yenye uhimili mkubwa wa
tani 35 kwa ekseli. Kwa hakika nchi yetu itasonga mbele kwa kasi na kuvuna
uchumi wa kijiografia ilionao.
Leo
tunashuhudia utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa sehemu ya kipande cha reli
ya kati kati ya Dar es Salaam na Morogoro chenye Kilometa 205 kati ya Kampuni
Hodhi ya Rasilimali za Reli na Ubia (JV) kati ya YAPI MERKEZİ İNŞAAT VE SANAYI
A.Ş. (Uturuki) MOTA-ENGIL, ENGENHARIA E na
CONSTRUÇÃO ÁFRICA, S.A. (Ureno). Gharama za mradi zitakua ni dola za kimarekani 1,029,900,000 ukiongeza
na kodi ya serikali dola za kimarekani 185,382,000 jumla kuu ni dola za
kimarekani 1,215,282,000. Kipande hiki ni sehemu ya
kwanza kati ya 5 ambazo zitatekelezwa hadi kufikia mwanza. Sehemu nyingine
ambazo zimetangazwa na zabuni zake zitafunguliwa mwezi wanne mwanzoni ni:-
a)
Morogoro hadi Makutopora 336Km (Sanifu-Jenga)
b)
Makutopora hadi Tabora 294Km (Sanifu-Jenga)
c)
Tabora hadi Isaka 133Km (Sanifu-Jenga)
d)
Isaka hadi Mwanza 248Km (Jenga)
IMETOLEWA NA:
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji,
RAHCO
Dar
es Salaam
03
Februari, 2017
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (Standard gauge) kutoka Dar es salaam hadi Morogoro unaotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano (sekta ya uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (Standard gauge) kutoka Dar es salaam hadi Morogoro unaotarajiwa kuanza hivi karibuni
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu Mhe.Profesa Richard Sigalla akizungumza katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (Standard gauge) kutoka Dar es salaam hadi Morogoro unaotarajiwa kuanza hivi karibuni
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,Masanja Kadogosa kwa kushirikina na Meneja wa Kanda ya Africa Mashariki,Murat Hasim na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Motaengil Africa,Manuel Antonio, wakisani mkataba wa ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (Standard gauge) kutoka Dar es salaam hadi Morogoro unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Bw. Masanja Kadogosa (kulia) na Meneja wa Kanda ya Africa Mashariki, Murat Hasim na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Motaengil Africa,Manuel Antonio wakibadilishana mikataba hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Bw. Masanja Kadogosa (kulia) na Meneja wa Kanda ya Africa Mashariki, Murat Hasim na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Motaengil Africa,Manuel Antonio wakiinyanyua juu mikataba hiyo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...