Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilichoko Kunduchi Dar es Salaam, Meja Jenerali Yacoub Mohamed, yuko nchini Kenya kwa ziara ya kikazi.
Kanali Mohamed amesema atatembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya kuona miundombinu yake na kubadilishana uzoefu na wakuu wa chuo hicho kilichopo Karen katika viunga vya jiji la Nairobi.
Mkuu huyo wa Chuo ametembelea Ubalozi wa Tanzania Nairobi na kuonana na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri. Lengo kubwa la ziara yake ni kubadilishana uzoefu na Chuo cha Ulinzi cha Kenya kuhusu uendeshaji na uandaaji wa mitaala.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi Talha Waziri (Kulia) akifurahia zaidi aliyokabidhiwa na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Meja Jenerali Yacoub Mohamed (wa pili kushoto). Kushoto ni Mshauri wa Kijeshi wa Ubalozi wa Tanzania, Kanali Fabian Machemba.
Meja jenerali Yavoub Mohamed na Kaimu Balozi (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja. Wa pili kulia ni Mshauri wa Kijeshi Kanali Machema na kulia ni Kanali Maulid Surumbu kutoka Chuo cha Ulinzi. Kushoto ni Kanali Njoroge wa Jeshi la Ulinzi la Kenya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...