Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama ametangaza mbio za kuelekea Tamasha la Pasaka ambalo linataraji kufanyika April 16 Mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Alex Msama amesema kuwa Tamasha hilo la kusifu na kuabudu,ambalo ni kubwa nchini kuliko matamasha yote litakuwa la aina yake katika mwaka huu wa 2017.
Msama amesema kuwa kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu itakuwa ni ''Umoja na upendo kudumisha amani ndani ya nchi yetu'' ,Lengo ikiwa ni kudumisha amani ndani ya nchi yetu  katika kipindi chote
 
“Napenda kuchukua fursa hii kuwaambia wapenzi wa muziki wa injili kuwa Msama Promotion imejipanga vyema kwa mwaka huu kuhakikisha kuwa inawaleta watu pamoja katika sehemu ambayo walikuwa wanaipenda ya kumtukuza mungu kila wakati wa pasaka kwa kuimba pamoja katika Tamasha la Pasaka wakiwa na wanamuziki maharufu wa muziki wa injili nchini”amesema Msama.

Msama ameweka wazi kuwa kutokuwepo kwa Tamasha la Krissmas kumezidi kuongeza ari ya watu kutaka kushiriki tamasha la Pasaka na kujionea mambo mbalimbali yanayolijumuisha tamasha hilo ambalo huandaliwa kwa umakini mkubwa.
 
Msama ametoa wito kwa wapenzi wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi katika Tamasha hili ili kuweza kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji. 
 
Amesema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu litafanyika katika mikoa mitano ili kuwapa fursa watu wa mikoani kushuhudia waimbaji wa nyimbo za injili na kusema kuwa tamasha hilo litaanza katika mkoa wa Dar es Salaaam.
 
Msama alimaliza kusema kuwa kwa sasa yupo katika hatua za kukamilisha vibali mbalimba vkiwemo vya Baraza Sanaa nchini (BASATA),yote hiyo ni kuhakikisha mambo yote yanakwenda katika mstari ulionyooka 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...