Ni siku moja tu imesalia kabla ya kutimia siku pendwa ya Wanamitindo wa hapa Tanzania ambao wanatarajia kukutanishwa kwenye Big Fashion Show ambayo hufanyika kila mwaka yaani  “Lady in Red”. 
Mwandaaji wa show hiyo Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin amesema kuwa show hiyo ni ya kipekee pia ina faida kubwa sana kwa wanamitindo chipukizi kwani Lady in red huwa inatoa kipaumbele kwa upcoming Designers kuonesha kazi zao jukwaani, hivyo mwaka huu  mambo yatakuwa mazuri sana ndani ya King Solomoni Hall”.
 Hivyo kwa wadau wote wapenzi wa mitindo mnakaribishwa  kuhudhuria usiku huo ili sanaa ya mitindo iweze kukua zaidi.
 Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin akiwa na wanamitindo wakiwa kwenye mkutano na wanahabari  akiongelea onesho la Lady In Red 2017 lililopangwa kufanyika kesho Jumamosi ndani ya ukumbi wa King Solomon Hall Namanga, Dar es salaam. 
 Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin akiwa na baadhi ya wanamitindo wakiwa kwenye mkutano na wanahabari  akiongelea onesho la Lady In Red 2017
Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin akiwa katika picha ya pamoja na badhi ya mamodo na wanamitindo wakiwa kwenye mkutano na wanahabari  akiongelea onesho la Lady In Red 2017

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...