
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Engorora,Akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkoa
Na Imma Msumba, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo Amefanya ziara katika Kijiji cha Engorora leo februari 14 na kujionea maendeleo mbalimbali hususani katika sekta ya Afya kijiji cha Engorora kilichopo Kata ya Kisongo.
Mh: Gambo akiwa kwenye ziara hiyo amekagua Kituo cha Afya kilichojengwa kijini hapo kwa nguvu za Wananchi ambapo Mkuu wa Mkoa Alisema,
" Nipende kuwapongeza wananchi wa kijiji hiki kwa kuweza kujitolea kwa nguvu zenu zote kwenye maendeleo ya kijiji hiki na Taifa kwa ujumla, Sisi kama Serikali inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli tumeamua kuchukua jukumu hili la kumalizia ujenzi wa Kituo hiki cha Afya,nipende tu kuwaambia wananchi wa kijiji hiki nitahakikisha kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, nitawaagiza watu wa Tanesco wajekuweka umeme kwenye zanahati hii,sambamba pia na watu wa Idara ya maji na wao pia wataleta huduma ya maji hapa haraka iwezekanavyo."
Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Vijijini kuhakikisha kabla ya mwisho mwezi huu anaonana Mwenyekiti wa Kijiji hicho na kuweza kuweka utaratibu wa kifedha juu ya swala la kumalizia ujenzi wa Kituo hicho kwa upande wa kuweka Tiles pamoja na kufunga milango ambayo ipo tayari mpaka sasa.
Pia mkuu wa Mkoa alimalizia kwa kuwapatia wananchi wa kijiji hicho saalamu za pongezi kutoka kwa Rais Magufuli
" Mh:Rais anawasalimia sana na pia anashukuru kwa kura zenu nyingi za ndio na kumuwezesha kuwa Rais wa awamu ya Tano."HAPA KAZI TU"
Wananchi wa Kijiji cha Engerora wakifuatilia Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa makini.
Baadhi ya Wawekezaji wa Kata ya Kisongo waliojitokeza kwenye kumsikiliza Mkuu wa Mkoa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...