Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo wikiendi hii alipata nafasi ya kutembelea nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine huko Monduli juu Wilayani Monduli.
Mh.Gambo alipata wasaaa wa kuzungumza na wajane wa kiongozi huyo mkubwa wa Kitaifa aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka 1984 eneo la Dumila huko Mkoani Morogoro, Mkuu wa mkoa alipata wasaa wakuzungumza na familia hiyo pamoja na wakazi majirani wanaozunguka familia hiyo na kusema maneno machache ambapo Alisema
"Kutembelea maeneo haya ambapo zipo kumbukumbu za mashujaa wetu waliolipigania Taifa letu kwa uzalendo mkuu, inatusaidia sisi viongozi vijana kuzirudia hadhiri zetu za uongozi ili tuweze kuwatumikia wananchi wanyonge kwa Uadilifu na uwajibikaji,ili kuacha alama katika nafasi tulizopewa na kuwatumikia wananchi kama walivyofanya wazee wetu hawa."
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,Akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...