Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo


Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa limewataka wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari zote katika kipindi hiki cha Masika. Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Omari Mkumbo alisema katika kipindi hiki cha mvua wananchi hawatakiwi kuvuka mito na mabonde yenye maji kwa hisia badala yake wanatakiwa wawe na subira.

“Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha katika kipindi hiki cha masika hamtakiwi kujipa ujasiri na kuyakadiria maji ya mvua hivyo zinahitajika tahadhari za kutosha dhidi ya watoto, au vyombo vyovyote vya usafiri kwani maji hayo huwa yanakwenda kwa kasi, yasubirini yapite acheni hisia ili kuhakikisha maisha yenu hayahatarishwi na mvua”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo.

Kamanda Mkumbo alitoa wito huo baada ya jana usiku kunyesha mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu na kusababisha vifo vya watu saba. Alisema katika tukio la kwanza jana Usiku wa saa 4:00 katika kijiji cha Kimbolo kata ya Enaboishu wilayani Arumeru, watu watano wote wakazi wa kijiji cha Kyoga walifariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Premio lenye namba za usajili T 579 BSG kusombwa na maji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...