Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imetiliana saini Mkataba wa ujenzi wa Bandari Kavu na Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la kujenga Taifa (Suma JKT), eneo la Kwala – Ruvu mkoani Pwani.

Mkataba huo wa zaidi ya shilingi bilioni 7.2 unaitaka Suma JKT kukamilisha bandari hiyo katika kipindi cha wiki Tisa kuanzia sasa ambapo tayari eneo la Hekta 500 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi huo utapunguza msongamano bandarini na katika jiji la Dar es salaam kwa kuwa magari mengi ya mizigo yanayokuja bandarini kuchukua mizigo sasa yataishia katika bandari hiyo.

“Mizigo itasafirishwa kwa njia ya reli kutoka bandarini kwenda Ruvu, hivyo magari ya mizigo hayatafika Dar es salaam na hivyo kupunguza msongamano”, amesema Waziri Mbarawa.Aidha, Profesa Mbarawa ameitaka Suma JKT kufanya kazi kwa uadilifu na kwa muda mfupi ili kuiwezesha mipango na mikakati ya Mamlaka hiyo kufanikiwa kwa urahisi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa amesema Mamlaka hiyo itaanza ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 300 katika bandari za Dar es salaam na Mtwara ili kuwezesha meli kubwa kuweza kutia nanga na kuongeza ufanisi wa Bandari nchini.“Upanuzi wa Bandari za Dar es salaam na Mtwara utavutia wasafirishaji wengi kutumia bandari hizi, hivyo wafanyakazi wote wa Mamlaka hii wafanye kazi kwa bidii na weledi”, amesisistiza Waziri Mbarawa.

Kwa upande wake Mwanasheria mkuu wa JKT, Kanali John Mbungo, amemhakikishia Waziri huyo kuwa kazi ya ujenzi huo itafanyika kwa ubora na katika kipindi kilichopangwa.Ujenzi wa Bandari Kavu katika eneo la Ruvu ni mkakati wa Serikali wa kupunguza msongamano katika jiji la Dar es salaam.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (Wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) kabla ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa bandari kavu baina ya TPA na Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT jijini Dar es salaam.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (Wa pili kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT Kanali John Mbungo, (Wa pili kulia), wakitiliana saini mkataba wa ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT Kanali John Mbungo (Kulia) wakikabidhiana mikataba ya ujezi wa wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani. Katikati ni Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuhudia makabidhiano hayo.
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Katikati), akisisitiza jambo kwa watendaji wa Mamlaka ya Bandari (TPA) mara baada ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani.

Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...