Picha na Fredy Njeje


Katika kuhakikisha vijana wanashiriki na kujikwamua katika mambo mbali mbali UNESCO  Youth Forum waliandaa semina ambayo ilihusu vijana kushiriki katika programu mbalimbali za umoja wa mataifa, Kudumisha amani kutoka ngazi ya vijana na jamii kwa ujumla ambapo Global Peace Foundation Tanzania walitoa mafunzo juu ya maswala hayo, kuhusu kusoma nje na kuelekezwa njia mbali mbali za kufanya kazi kwa kujitolea katika asasi mbalimbali za kiraia.


Akizungumza na vijana hao kutoka vyuo mbalimbali na wale ambao walimaliza vyuo mwakilishi wa    asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini Tanzania Bi. Anna Mwalongo alisema kuwa Global Peace Foundation ni Taasisi isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile ina makao yake makuu  katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.” Alisema Anna.


Aliongeza kuwa Mnamo mwezi wa saba mwaka 2015 Global peace foundation waliandaa Mkutano mkubwa wa amani uliofanyinka Zanzibar uliojulikana kwa jina la Global peace Leadership Conference (GPLC Zanzibar) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais Mh. Balozi Seif Ali na kuhudhuriwa na marais wastaafu kutoka nchi mbalimbali. 

 "Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendesha kampeni ya “AMANI KWANZA” ambapo aliwalenga wanawake na vijana kushiriki katika uchaguzi huo kwa amani, alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa GPF wanampango wa kupanua wigo zaidi ili kuwafikia watanzania wengi zaidi kueleza mambo mbalimbali ya amani kupitia kampeni yao ya “VIJANA NA AMANI” " Alisema Anna


Kwa upande wake Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa uelewa ili wapate kujiunga.

Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship' katika zinazotolewa sehemu mbalimbali.
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia  Global Peace Foundation (GPF) Tanzania aliyewakilisha katika Semina hiyo Bi. Anna Mwalongo akielezea kwa kifupi kuhusu Asasi hiyo.
Mshauri wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi  Bw. Anthony Luvanda akitoa masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali.
Baadhi ya vijana wakiendelea kusikiliza kwa makini mambo mbalimbali katika Semina Hiyo
 Watoa Mada wakiwa pamoja na Baadhi ya washiriki waliohudhuria Semina hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...