Teresia Mhagama na Zuena Msuya,
Arusha
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na
Mbunge wa Simanjiro, James Millya wametembelea Kituo cha Jimolojia Arusha,
unapofanyika Mnada wa Pili wa Kimataifa kwa madini ya Tanzanite ili kujionea
jinsi mnada husika unavyoendeshwa.
Mnada huo wa kimataifa
unaofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 9 hadi 12, Februari, 2017 unahudhuriwa
na wanunuzi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na wauzaji kutoka ndani ya
nchi.
Akitoa maelezo kuhusu mnada huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha
Uthaminishaji Madini katika Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard
Kalugendo, alisema kuwa lengo la mnada huo ni kuhakikisha kuwa madini ya
Tanzanite yanapata soko rasmi na Serikali kupata mapato yake stahiki.
Mkurugenzi wa Kitengo cha
Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini
(TANSORT), Archard Kalugendo,(wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo (wa Tatu kushoto) na Mbunge wa Simanjiro, James Millya (wa kwanza kulia)
mara walipotembelea Kituo cha Jimolojia Arusha unapofanyika Mnada wa Pili wa
Kimataifa kwa madini ya Tanzanite ili kujionea jinsi unavyoendeshwa.Wa kwanza
kushoto ni mmoja wa wakurugenzi wa Mgodi wa Tanzanite One, Faisal Shahbhai.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Watumishi kutoka Wizara ya Nishati na
Madini wakiangalia jinsi wanafunzi katika Kituo cha Jimolojia jijini Arusha wanavyojifunza
namna ya kukata madini ya vito na kuyaweka katika maumbo ya kuvutia. Kituo
hicho cha Jimolojia kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Mkurugenzi wa Kitengo cha
Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini
(TANSORT), Archard Kalugendo,(wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Baadhi ya
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Watumishi kutoka
Wizara ya Nishati na Madini kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Kituo cha
Jimolojia jijini Arusha ambacho kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo (katikati) akizungumza na mmoja wa wanunuzi wa madini ya Tanzanite katika
Mnada wa Pili wa Kimataifa wa Madini hayo unaofanyika jijini Arusha. Wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito,
katika Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo na wa kwanza
kulia ni mmoja wa wakurugenzi wa Mgodi wa Tanzanite One, Faisal Shahbhai.
Mkurugenzi wa Kitengo cha
Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini
(TANSORT) Archard Kalugendo, (katikati)
akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge
wa Simanjiro, James Millya (wa kwanza kulia) waliotembelea mnada wa Pili
wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite
jijini Arusha. Wajumbe hao ni Mhe. John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini
(CHADEMA), (wa kwanza kushoto), Mhe. Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalum
(CCM),(wa pili kushoto), ) na Mhe.
Dunstan Kitandula Mbunge wa Mkinga (CCM)
(wa pili kulia). Wengine katika picha ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya
Kaskazini, Adam Juma (wa Tatu kulia) na Kaimu Mratibu wa Kituo cha Jimolojia
cha Arusha, Erick Mpesa (wan ne kulia).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...