Tumesikia mara kadhaa
wazazi wakigombania kukaa
na mtoto/watoto. Haya
hujitokeza baada ya
kuvunjika kwa ndoa
kwa talaka, baada
ya kutengana bila
talaka au pasi
na ndoa wazazi
tu wamezaa na
sasa hawaelewani na
mgogoro wa nani
akae na mtoto
umeibuka.
Tunahitaji kujua ikiwa
kuna haja ya
kugombania mtoto kwa matusi na
ugomvi wakati zipo
taratibu za kisheria. Tujue kama yafaa
kutumiana jumbe chafu
za kudhalilishana pale unapotaka
ukae na mtoto. Jibu
ni hapana ila
ni watu tu
wajue taratibu.
Ifahamike kuwa iwe
kwa ndoa au
bila ndoa haki
ya mtoto kukaa
na wazazi au
mzazi iko kwa yeyote.
Ni aidha
atakaa na wote wawili
au mmoja wao. Sheria
namba 21 ya 2009, Sheria
ya Mtoto ndiyo
sheria ambayo kwasasa
inasimamia ustawi na
haki za mtoto.
Hivyo makala yataeleza
yaliyo katika sheria
hii.
1.MTOTO NI
NANI.
Kifungu cha 4( a )
cha sheria ya
mtoto kinatafsiri neno
mtoto kumaanisha mtu
ambaye yuko chini
ya umri wa miaka
18. Kwa maana hii
miaka 18 kamili
sio mtoto isipokuwa sasa chini
yake ndiye mtoto
kwa tafsiri ya
kifungu hiki.
Sambamba na hilo kifungu
cha 7( 1 ) kinaeleza haki
ya mtoto kukaa
na wazazi wake
wote wawili. Basi yaje
hayo ya kutengana
na mtoto kuishi
maisha ya mzazi mmoja , bado
uhalisia ni haki
ya msingi ya
mtoto kukaa na
wazazi wake wawili
kama ilivyoainishwa hapa.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...