Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameziagiza Halmshauri zote za mkoa huo kuhakikisha kuwa zinatenga asilimia tano ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake.

Agizo hilo lilitolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani humo jana. Ndikilo alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.

“Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo hazitatekeleza wajibu wahakikishe wanajitahidi kufanya jukumu hilo muhimu kwa maendeleo ya wanawake wa mkoa huo” alisema Seneda.

Alisema katika kuwawezesha wanawake kiuchumi, Serikali imeanzisha Benki ya Wanawake Tanzania, mifuko mbalimbali ukiwemo mfuko wa maendeleo ya wanawake (WDF) pamoja na kuhamasisha uanzishaji wa Saccos, vikundi vya uzalishaji mali na Vicoba na kwa kupitia fursa zilizopo kuwawezesha wanawake wajasiriamali kupata mikopo yenye masharti nafuu.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Seneda akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 61,550 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wilayani humo iliyotolewa na Benki ya NMB.
Wadau wa maendelea wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo baada ya kukabidhi msaada wa magodoro na vifaa vingine vyenye thamani ya sh.700,000.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness William Seneda (katikati), akihutubia kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani Kisarawe jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga’alo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...