Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo mchana jijini Dar kuhusiana na maendeleo ya maandalizi ya tamasha la pasaka linatlotajia kuanza hivi karibuni.
Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii.
Tamasha
kubwa la muziki wa injili linalofahamika kama "Tamasha la Pasaka" sasa kufanyika
katika uwanja wa Uhuru april 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mratibu wa Tamasha hilo, Alex Msama
amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na sasa uwanja wa uhuru ndio sehemu
maalum ya kufanyia Tamasha hilo.
“Malengo ya
tamasha la pasaka ni yaleyale ni kuliombea taifa na kumuombea Rais wa nchi Dkt
John Pombe Magufuli ili aendelee
kutawala kwa amani katika taifa hili” amesema
Ametaja kuwa
tamasha hilo kwa sasa litatembea katika mikoa kumi na kufanya uzinduzi wa
albamu mbili



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...