Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba amewataka maofisa na askari Polisi kote nchini kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu ili kujenga taswira nzuri kwa wananchi wanaowahudumia jambo ambalo litaongeza imani na ushirikiano katika kukomesha vitendo vya uhalifu nchini.
Waziri Nchemba ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha Maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kutoka makao makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na vikosi kutoka bara na Zanzibar kinachoendelea mkoani Dodoma.
Alisema Pamoja na Jeshi hilo kufanya kazi nzuri bado linakabiliwa na changamoto ya baadhi ya askari na maofisa wasio waadilifu wanaofanya vitendo vya kuwabambikia wananchi kesi na wakati mwingine kuwabadilishia kesi ili kujenga mazingira ya kupatiwa rushwa jambo ambalo ni kinyume na maadili ya askari Polisi.
“Fanyeni kazi kwa weledi hasa kwa kuwasimamia waliopo chini yenu kwa kuwa wapo baadhi yao bado hawataki kubadilika na katika awamu hii lengo letu ni kutoa haki kwa maskini hivyo ninyi kama wasimamizi wa sheria mnapaswa kutenda haki mnapofanya kazi zenu na wale wasiotaka kubadilika hamna budi kuchukua hatua ” Alisema Nchemba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) pamoja na
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu wakiongozwa na askari wa
kikosi cha bendera kuingia ukumbini kwa ajili ya ufunguzi wa kikao kazi cha
mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa
mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi
la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akitoa
hotuba ufunguzi wa kikao kazi cha mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa
jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma.
Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akiongea na
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu wakati wa hafla ya ufunguzi wa
kikao kazi cha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi
kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Baadhi ya maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa maadili ya afisa
wa polisi wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa hao na
makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan
Mndeme-Jeshi la Polisi. Picha Na Hassan Mndeme.
HABARI ZAIDI SOMA HAPA
HABARI ZAIDI SOMA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...