Na
Hassan Silayo
Mwenendo
wa somo la Kiswahili nchini umeendelea kuimarika na hii ni kutokana na jitihada
mbalimbali ziliwekwa na serikali katika somo hilo.
Akitoa
ripoti matokeo ya utafiti wa Uwezo,Meneja wa Uwezo Tanzania Zaida Mgalla
alisema kuwa kwa watoto walikuwa darasa la tatu walioweza kufauli majaribio ya
Kiswahili mwaka 2011 walikuwa asilimia 29 tofauti na asilimia 56 ya mwaka 2015.
Bi.
Zaida Aliongeza kuwa kwa darasa la saba kumekuwa na ongezeko la watoto
kujifunza na kufanya vizuri zaidi ikiwa kwa mwaka 2011 asilimia 76 walifaulu
majaribio ya Kiswahili ikilinganishwa na asilimia 89 ya mwaka 2015.
“Tunaipongeza
Serikali ka jitihada zake za kuhakikisha watoto wanapiga hatua katika somo la
Kiswahili tunaona ongezeko la ufaulu limeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka
na hii inatia moyo na serikali inatakiwa
iendelee kuweka jitihada katika kimarika zaidi na kuacha kuridhika na matokeo
haya”.Alisema Zaida.
Aidha
Zaida aliongeza kuwa Taarifa ya Tafiti ya Uwezo inaonesha kuwa uwiano kati ya
Wanafunzi na vitabu umeendelea kuboreka kutoka wanafunzi 30 kutumia kitabu
kimoja mwaka 2013 hadi wanafunzi 8 kwa mwaka 2014, hadi kufikia wanafunzi 3
kutumia kitabu kimoja kwa mwaka 2015.
Akiongelea
kuhusu ufaulu katika somo la Kiswahili Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan
Eyakuze alisema kuwa inatia moyo kuona
watoto wetu wanapata matokeo mazuri zaidi kuliko miaka ya nyuma kwenye somo la
Kiswahili.
Wakichangia
mijadala katika halfa hiyo baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wameishauri serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri ya watoto
kufanya vizzuri katika masomo pamoja na kuboresha maslahi ya walimu ili
kuwajengea morali katika kufundisha.

Meneja Uwezo Tanzania Zaida Mgalla akiongea na wageni waalikwa wakiwamo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa hafla ya utoa wa matokeo wa Tafiti za Uwezo ambapo mbali na changamoto nyingine takwimu mpya za uwezo zinaonesha mwenendo mzuri katika somo la Kiswahili na uwiano mzuri uliopo kati ya wanafunzi na vitabu,Leo Mjini Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Seleman Jafo akiongea na wageni waalikwa wakiwamo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa hafla ya utoa wa matokeo wa Tafiti za Uwezo ambapo alipongeza tafiti za TWAWEZA na kuwataka watendaji serikalini kuzitumia tafiti hizo ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya elimu,Leo Mjini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...