Kaimu Mrajisi wa Vyama vya ushirika nchini, Tito Haule amevitaka vyama vyote vya Ushirika nchini kujiepusha kujiingiza kwenye mikopo isiyokuwa na tija kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha, ambayo inavighalimu vyama hivyo na kushindwa kujiendesha kutokana na kuzidiwa na madeni ambayo hayaendani na uwezo halisi wa vyama husika na kuwaingiza wanachama wao katika matatizo kutokana na kushindwa kulipa madeni hayo huku akiwashauri kuangalia huduma ambazo zinawalenga wananchi moja kwa moja.

Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati wa kusaini makubaliano na Benki ya Wanawake ya Covenant ambayo yataiwezesha benki hiyo kuweza kutoa huduma mbalimbali za bima pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kwa vyama mbalimbali vya ushirika nchini, Katika hafla hiyo iliyofanyika mkoani Dodoma Mrajisi ameitaka benki hiyo kuhakikisha inatimiza adhma ya kutoa huduma ambazo zitawanufaisha wanachama moja kwa moja na sio viongozi wachache.

“Vyama vingi vimekuwa na mazoea ya kujiingiza katika mikopo mikubwa na wakati mwingine hata kuzidi uwezo halisi wa vyama husika, lakini pia viongozi wanaokuwepo wanakuwa sio waaminifu na kujikuta wanashindwa kusimami matumizi ya fedha hizo kwa uaminifu na kujikuta wanaviingiza vyama katika matatizo makubwa,” alisema Haule na kuongeza kuwa, “Ninawsaihi viongozi waache utaratibu huu ambao umeendelea kuvifanya vyama vya ushirika kushindwa kuwa sehemu ya ukombozi wa wanachama wake bali sehemu ya kuwakandamiza,”

Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Tito Haule (Katikati) Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, Wakitia saini mkataba utakao iwezesha Covenant bank kutoa huduma mbalimbali za bima kwa vyama vya ushirika nchini, waliosimama ni kutoka kushoro ni, Mwanasheria wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Angela Chilewa, Meneja Uendeshaji wa Covenant Bank, Baraka Enock pamoja na Mwanasheria wa Benki hiyo Hadija Sijaona. Aliyeketi ni Kaimu Naibu Mrajisi Udhibiti na Usimamizi, Collins Nyakunga.
Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Tito Haule (Katikati) Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, Wakitia saini mkataba utakao iwezesha Covenant bank kutoa huduma mbalimbali za bima kwa vyama vya ushirika nchini, waliosimama ni kutoka kushoro ni, Mwanasheria wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Angela Chilewa, Meneja Uendeshaji wa Covenant Bank, Baraka Enock pamoja na Mwanasheria wa Benki hiyo Hadija Sijaona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...