Benki ya Dunia kupitia washirika wake wa Maendeleo imeamini ya kuridhika na hatua kubwa iliyochukuliwa na Jamii ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar katika kusimamia miradi yao kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania{TASAF} Awamu ya Tatu katika kujiondolea Umaskini.
Viongozi wa Ujumbe wa Washirika hao wa Maendeleo ulitoa kauli hiyo wakati ukitoa tathmini ndogo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua miradi ya Jamii inayotekelezwa kupitia Tasaf Tatu katika maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini Unguja na Pemba.
Kiongozi wa Ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdulah alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ziara ya Ujumbe wake imeshuhudia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Jamii kutokana na kundi kubwa la Wananchi lilivyoamua kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi yao waliyoianzisha.
Bwana Moderes alisema Zanzibar imeonyesha mfano bora katika uendelezaji wa miradi ya Maendeleo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} awamu ya Tatu kiasi kwamba Uongozi wa Benki ya Dunia kupitia Washirika wake imefurahia hatua hiyo ya mafanikio.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...