Na Tiganya Vincent-Kaliua
18.5.2017

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiako wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Celestine Mushi ametoa wito kwa 
Mashirika Kimataifa na Umoja wa Ulaya kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwasaidia atanzania wapya (waliokuwa wakimbizi wa Burundi) kuhakikishwa anaunganishwa na jamii ya Watanzania mara baada ya kupata uraia.

Balozi Mushi ametoa kauli hiyo jana katika eneo la Ulyankulu wilayani Kaliua wakati alipokuwa na Ujumbe wa Mabalozi kutoka Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ikiwemo Uingereza.

Alisema kuwa baada ya Serikali kuwapatia waliokuwa baadhi ya wakimbizi wa Burundi Uraia ni vema nchi hizo na Mashirika ya Kimataifa yakasaidia kuongeza raslimali mbalimbali ambazo zitaisaidia Serikali iweze kuwaunganisha vizuri raia hao wapya na raia wengine hapa nchini.

Balozi Mushi aliongeza fedha za Serikali pekee hazitoshi kukamilisha zoezi la kuwaunganisha raia hao kwasababu yapo mahitaji ya wananchi mengine hapo nchini yanayotegemeza hizo fedha kidogo inazokusanya kutokana na vyanzo vyake mbalimbali vya mapato na hivyo ni vema nao wakasaidia kwa upande wao.

Alisema kuwa kimsingi raia hao wapya wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama, uhaba wa vifaa tiba, zahanati , kutokuwa na miundombinu ya kutosha ya elimu na kukosa elimu ya kutosha kuhusu uzazi wa mpango.

Alisema kuwa kukosekana kwa elimu ya kutosha kumewafanya wakazi hao wawe na familia kubwa ambazo hawawezi wakati mwingine kuziwezesha katika huduma za jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...