Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mh Martha Mkupasi ameongoza wakazi wa Mbogwe kwenye Zoezi la Usafi wa Mazingira kwa kufanya usafi eneo la Kituo cha Afya Masumbwe na maeneo yanayozunguka kituo hicho.

Akiongea na wananchi baada ya zoezi la usafi, mh Mkupasi amewataka wananchi kujijengea tabia ya kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka kila siku na wasisubiri mwisho wa mwezi kwani kwa kupenda usafi itawasaidia kujiepusha na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Pia amewasisitiza wananchi kutunza mazingira na kuepuka kukata miti ovyo badala yake wapande miti ya kutosha .

Pamoja na hayo mh Mkupasi aliongea na Vijana wa Kikundi cha Scout walioungana na wananchi kwenye zoezi la usafi , nakuwahimiza kupenda masomo yao ya kila siku na kuweka bidii kwani bila elimu hawezi kutimiza ndoto zao .

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Afisa Mazingira wa Wilaya Charles Karibu Tuyi aliwashukuru wananchi na kikundi cha scouti kwa kujitolea kuja kufanya usafi wa mazingira kwenye kituo cha afya Masumbwe na kuwahimiza kuendelea kusafisha mazingira wanayoishi na kuwataka waepuke kutupa uchafu kwenye mitaro kwani utupaji wa taka ngumu unaweza kuziba mitaro na kusababisha mafuriko .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...