Mhandisi wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya kifaa cha kupima mvua kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea vituo hivyo vinavyotekelezwa na Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari uliopo Lushoto Mkoani Tanga Juni 6, 2017.
Mhasibu Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Consolata Mazigo akiuliza swali kwa Mhandisi wa mitambo ya hali ya hewa Bw. Michael Minja wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 6, 2017 Lushoto Tanga.
Mhandisi wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya mtambo wa kisasa wa usomaji wa taarifa za hali ya hewa kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari ulio chini ya Ofisi hiyo.
Baadhi ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakinukuu maelezo ya Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Pangani Bw. Vendelin Basso (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kutathimini Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo Kilimanjaro, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Moshi Juni 7, 2017.
Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Mto Pangani Bw. Vendelin Basso akiwasilisha utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari kwa upande wa Bonde la Mto Pangani mkoani Kilimanjaro wakati wa ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi huo uliofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 7, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...