Na Abraham Ntambara. 
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye. 
 Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12.
 “Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais. 

Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu mengine. 
Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan bendera ikiwa ni ishara ya kumpatia ulezi wa chama hicho katika hafla iliyofanyika, kwenye viwanja vya Jumba la Makumbusho Dar es Salaam leo. 
Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA
Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu.

Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi
Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA


Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides

Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...