UONGOZI wa timu ya mpira wa miguu ya Everton kutoka nchini Uingereza imeridhishwa na huduma inayotolewa kwa wagonjwa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo mabusha na matende hapa nchini. 
Hayo yamezungumzwa na mmoja wa viongozi wa Everton Bw. Darren Griffiths ambao ni washiriki katika kuchangia huduma ya magonjwa hayo hapa nchini ambaye ameongozana na timu yake ili kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Gor Mahia kutoka chini Kenya.
“Tunayo furaha kuona wagonjwa wengi waliokuwa wanaumwa mabusha na metende nchini Tanzania kwa sasa wamepona kabisa na tunahaidi kuwa na Wizara ya afya bega kwa bega katika kutokomeza magonjwa haya” alisema Bw. Darren Griffiths
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt. Vida Mmbaga amesema kuwa kutokana na ushiriki wa Everton katika kuchangia utoaji wa Huduma ya kutibu ugonjwa huo wamefanikiwa kupata ujuzi wa upasuaji hasa kwa wagonjwa wa mabusha na matende hapa nchini.


Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Vida Mmbaga akisisitiza juu ya baadhi ya juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya viongozi kutoka timu ya Everton na mwakilishi kutoka Liverpool katika zoezi lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
Mratibu wa Mpango wa Taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo Mwingira akibadilishana Mawazo na Mwakilishi kutoka Liverpool wakati wa tukio la kusaidia waliokuwa wagonjwa wa mabusha na matende liliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii. 
Mmoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza na aliekuwa mchezaji wa timu hiyo Leon Osman akigawa zawadi kwa waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi la kuwasaidia lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
Picha ya pamoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza, Viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi lakuwasaidia lililofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...