Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Usalama barabarani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akizungumza leo baada ya kufanya ukaguzi amesema kuwa hakuna basi linaweza kuondoka katika kituo cha mabasi bila kufanyiwa ukaguzi.
Samwix amesema kuwa basi ambalo likibainika katika kituo cha Mabasi Ubungo lina makosa haliwezi kufanya safari zake ambapo amewataka wamiliki kufanya matengenezo ya mara mara ili kuondokana na adha ambazo watakuna nazo mara baada kufanya ukaguzi wa mabasi hayo.
Aidha amesema kuwa madereva wanatakiwa kuwa mabalozi wa kukataa kufanya safari zao pale wanapobaini kuwa basi lina ubovu wowote ili kupukana na ajali ambazo zinatokana na ubovu wa mabasi hayo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...