Na Mathias Canal, Zanzibar
Kongamano la nne
la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference)
limefunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 kwa kuwashirikisha washiriki wapatao
350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wamehudhuria zaidi ya 200 na watendaji
kutoka taasisi za Serikali zote mbili wakiwa ni 150.
Diaspora
wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini katika sekta ya
kuimarisha na kuanzisha viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuifanyaTanzania
kuwa nchi ya viwanda.
Kauli hiyo
imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa
Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi litakalodumu kwa siku mbili
Agosti 23 na 24, 2017 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel uliopo katika kijiji cha
Kama Wilaya ya Magharibi A.
Mhe Makamba
alisema kuwa kwa sasa Demokrasia imeimarika nchini kutokana na serikali kupitia
vyombo vyake vya ulinzi na usalama kukubaliana kwa kauli moja kuimarisha usalama
wa wananchi ili kurahisisha uimara wa uwajibikaji wa ujenzi wa Taifa.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB)
akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya
nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Ndg Geofrey Mwambe akizungumza wakati wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni linalofanyika Sea Cleaf Hotel Mjini Zanzibar
Washiriki wa
Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakitembelea shamba la BIG BODY SPICE kujionea kilimo cha mazao ya viuongo
Washiriki wa
Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa
makini maelezo kuhusu kilimo cha mazao ya viuongo mara baada ya kutembelea shamba la BIG BODY SPICE
Washiriki wa
Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa
makini maelezo kuhusu kilimo cha mazao ya viuongo mara baada ya kutembelea shamba la BIG BODY SPICE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...