“Napenda kuwapongeza GHACOF kwa kuwezesha sayansi ya hali ya hewa kutumika katika shughuli za maendeleo ya jamii, nikiangalia kwa upande wa nchi yetu ya Tanzania kumekuwa na ongezeko la mahitaji na matumizi ya huduma za hali ya hewa kwa kiasi kikubwa sambamba na wigo mpana wa uelewa wa matumizi ya taarifa hizo, ambapo inasaidia sana wananchi kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa,” haya aliyasema Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) wakati akifungua rasmi Mkutano wa 47 wa maandalizi ya utabiri na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika (Forty Seventh Greater Horn of Africa Climate Outlook Forum (GHACOF-47) kwa msimu wa mvua za vuli wa mwezi Oktoka hadi Desemba 2017.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB)
katika picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa Mkutano wa 47 wa maandalizi
ya mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa msimu wa mvua za vuli (Oktoba-Disemba
2017) kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika (Greater Horn of Africa
Climate Outlook Forum-GHACOF-47), Zanzibar Beach Resort, tarehe 21-22 Agosti
2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...