TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imefanya mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara.
Katika mhadhara huo msemaji Mkuu alikuwa Prof. Brian Van Arkadie, majadiliano yalitanguliwa Prof Samuel Wangwe na Aloyce Hepelwa
Akiwasilisha mada yake aliwataka wataalamu kubadilika katika namna ya kusaidia kuongeza tija katika kilimo na kuachana na dhana za zamani kwamba wakulima wameshindwa kubadilika na kukwamisha maendeleo.
Amesema katika mjadala huo wa hadhara kuhusu maendeleo ya kilimo kutoka wakati wa uhuru hadi sasa katika jengo la mikutano la ESRF mjini hapa alisema kwamba tafiti nyingi zimekuwa zikishutumu wakulima kwa kuwa na muono mdogo na kubisha mabadiliko yanayohitaji kuongeza uzalishaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...