Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani
amesema kuanzia Agosti 30 mwaka huu, Serikali itatangaza zabuni ya kuanza ujenzi
wa Mradi Mkubwa wa Umeme wa megawati 2100 katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji
mkoani Pwani eneo la Stiegel’s Gorge
Akizungumza jijini Dar es Salaam Dkt. Kalemani amesema, taratibu za awali zimeshaanza ambapo
wataalaumu wa ndani na nje wameshakutana
na kuchagua sehemu za kujenga mradi huo katika Mto Rufiji, ambapo tayari
Shirika la Umeme Nchini ( Tanesco ) limeanza upembuzi yakinifu wa kujenga
miundombinu ya umeme na Wakala wa barabara nchini (Tanroad) kujenga miundombinu ya barabara.
Ujenzi wa mradi wa umeme wa megawati 2100 kutoka maporoko ya
maji ya Mto Rufiji Mkoani Pwani ( Stiegler’s Gorge)unatarajiwa kuanza ndani ya
kipindi cha miezi miwili ijayo baada ya
taratibu za zabuni kukamilika, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard
Kalemani amewambia watanzania kuwa, tayari Serikali imetenga fedha za
kutekeleza mradi huo, na hatua za awali za utekelezaji zimekwisha fanyika,
ambapo tarehe 30 ya mwezi huu wa Agosti
Serikali itatangaza zabuni kwa wakandarasi wa ndani na nje ya nchi ili waweze
kuomba kufanya kazi .
Dkt. Kalemani amesema mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga
mradi huo ni yule tu atayeridhia kujenga kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi
zaidi ya uliowekwa Pia Dkt. Kalemani anatoa ufafanuzi namna ambavyo Serikali imejiandaa
katika kutekeleza mradi huo.
Kwa mujibu wa Dkt Kalemani, mradi huo
utakapokalimilika utakasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme
nchini na kwamba Serikali haitarajii
kuongeza bei ya umeme.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akishuka kwenye boti kwa ajili ya kuelekea kwenye eneo la Stieglers Gorge kutakapojengwa mradi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...