Soka la nchi yetu linaenda 'halijojo' halina mtiririko wenye mwendelezo makini.Tangu kuanzishwa kwa Taifa hili ni Mara moja tu nchi yetu ilishiriki michuano mikubwa kwa ngazi ya Afrika yaani Afcon.
Ilikua mwaka 1980 ambao tulinyanyaswa sana katika uwanja wa Sululele pale Nigeria. Sululele ndio mtaa aliozaliwa msanii nguli wa Nigeria Wizkid,na anatanbulika kama mfalme wa Sululele.
Vizazi Vingi vimepita tangu mwaka 1980 hadi sasa. Na imekua kama ni suala la kawaida kila nyakati zimekuwa zikilalamikiwa. Na nyakati zikipita waliolalamikiwa kwa viwango vyao nao wanawalalamikia wale wanaocheza kwa wakati ambao waliolalamikiwa hawachezi.
Imekua kama mbio za 'relay' kila mlalamikiwa muda ukimwacha nae husubili wa kumlalamikia. Leo twaweza kuwa na kiwango kizuri tikaridhisha mashabiki lakini kesho tunakuwa kawaida.
TUFANYE HAYA KUNUSURU SOKA LETU.
Katika masuala ya utafiti kuna jambo linaitwa kukusanya taarifa za jambo la utafiti.Pia unatakiwa kufanya mapitio ya maandishi ili kujua tatizo uchunguzalo kama limewahi kuchunguzwa. Baada ya kuchunguza unatazama kufanikiwa au kutofanikiwa kwa utafiti huo.
Katika soka tinapaswa kutumia utafiti wa wenzetu walioporomoka kisoka na wakarudi vyema. Iko mifano mingi lakini tuwatazame Wajerumani na Wabelgiji.
Katika nchi ya Ujerumani baada ya kufanya vibaya katika michuano ya Ulaya mwaka 2000 walirudi katika vitalu 'grassroots' vya soka.
Wataalamu elfu moja walisambazwa nchi nzima kutafuta vipaji vya soka. Wataalamu hao wenye elimu ya ukocha waliingia miji mbali na maeneo ya chini kabisa kufanya kazi hiyo.
Maamuzi ya kuingia vitaluni kusaka vipaji ilitokana na jicho lao kuona hawana ubabe tena Ulaya.Maeneo ya Gelsenkirchen, Bremen, Colony, Munich,Hamburg, Wolfsburg, Frankfurt,Stuttgart yalifikiwa na wataalamu hao.
Uhai wa Ujerumani ulibaki katika vilabu vyao ambapo Mwaka 2001 Bayern Munich walichukua kikombe cha ubingwa wa Ulaya. Mwaka uliofuata klabu ya Bayer Leverkusen walicheza fainali dhidi ya Rael Madrid. Mwaka 2002 wakapoteza fainali dhidi ya Brazili pale Yokohama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...