
Akzungumza na mwandishi wetu baada ya kuisha mkutano wa wanachama kutoka Tanga, msemaji wa klabu hiyo maarufu Wagosi wa Kaya, Hafidh Kido alisema kwa mipango iliyokuwepo hakuna sababu ya kuifanya timu hiyo kongwe nchini kushindwa kurejea ligi kuu msimu ujao.
“Mkutano ulikuwa na ajenda nyingi lakini kubwa ilikuwa ni kuleta umoja na kubainisha mikakati ya kushiriki vema ligi daraja la kwanza msimu huu.
“Tumefanya usajili wa nguvu, wachezaji wengi waliokuwa wakishiriki ligi kuu msimu uliopita tumewanaka na tayari wamesharipoti kambini,” alisema Hafidh Kido na kuongeza:
“Hii ni Coastal Union mpya, wapenzi na wanachama wote uliokuwa ukiwajua wamerejea kwa ajili ya kuongeza nguvu. Sasa hivi Coastal Union ni wali ng’ombe hakuna njaa.”
Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Usajili na Mashindano, Hemed Hilal ‘Aurora’ alisema; “Makundi ndiyo yaliyoidhoofisha Coastal Union lakini leo nathibitisha wazi makund yamekufa na Coastal Union ni moja.”
Alisisitiza kuwa kila mmoja atimize wajibu wake ili msimu huu mambo yanyooke na Coastal Union irudi mahali panapostahili kwa sababu kushiriki ligi daraja la kwanza si hadhi yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...