Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
Uchumi wa kati na uchumi wa viwanda unatokana na kuwepo kwa rasilimali watu yenye ujuzi na maarifa wa kufanya kupata matokeo hayo.
Hayo ameyasema Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati wa kuwaaga watumishi wa tano wa Wizara ya Fedha na Mipango kusoma shahada za pili katika vyuo vikuu vya Uingereza kwa Ufadhili wa Uingereza , amesema kuwa vijana wanaokwenda huko watafanya vizuri na kuleta maarifa nchini katika masuala mbalimbali katika wizara ya Fedha.
Amesema Wizara ya Fedha na Mipango ndio moyo wa nchi hivyo kupata ufadhili kwa vijana hao watakuwa ni msaada kwa wizara katika kufanya masuala mbalimbali.
Nae Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kuwa Uingereza imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika maendeleo ya Tanzania na kuamua kutoa ufadhili kwa watumishi watano ni fedha nyingi ya walipakodi wa Uingereza.
Amesema kuwa katika hatua ya kupata ufadhili huo wakirudi watafanya kazi katika masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya uchambuzi wa bajeti.Dk. Mpango amesema watumishi wengine wajiandae na ufadhili kutokana na mahitaji yaliyopo kwa watumishi wa wizara hiyo.
Watumishi hao ni Herieth Lubinga, John Kabiti, Gloria Mduda,Peter Kalugwisha pamoja na Susan Mbwayuwayu.
Waziri wa Fedha na Mipango , Dk. Philip Mpango akizungumza wakati wa kuwaaga watumishi wa wizara fedha wanaoenda kusoma vyuo vikuu vya Uingereza kwa ufadhili wa nchi Uingereza.
Mmoja wa Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya Uingereza, John Kabiti akizungumza juu ufadhili leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza juu ya vijana wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya Uingereza kwa ufadhili wa nchi Uingreza.
Picha ya Pamoja katika mawaziri na watumishi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya Uingereza kwa ufadhili nchi ya Uingereza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...