Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa waalimu katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama Manispaa ya Kinondoni.
Mafunzo hayo kwa waalimu yameanza kufuatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua application mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa kutumia technologia za kisasa.
Akiongea kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema,
‘Hapo awali tulikuwa tumeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi lakini tumeona ni bora na waalimu wa hapa shule hii Kijitonyama nao waanze kupata mafunzo. Hii itasaidia kwani kwa baadae ndio watakaokuwa wakitoa mafunzo kwa wanafunzi na hii itatupa nafasi ya kuendelea kuwezesha shule zingine.
Waalimu wamepokea hatua hii kwa furaha na wanao hamasa kubwa kwenye mafunzo. Hii inathibitisha nia ya kampuni ya Airtel ya kutoa fursa kwa kila Mtanzania, aliongeza Matinde.
Meneja Matukio wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam leo.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam leo.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam leo/
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...