Afisa Usimamizi na Ubora wa hospitali ya Amana, Lucy Mbusi (kushoto) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa tiba na dawa kwa hospitali ya Amana, jijini Dar es salaam, vilivyotolea na Benki ya DTB kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti", mwishoni mwa wiki. Katikati ni Muanzilishi wa Doris Mollel Foundation inayojishughulisha na kusaidia watoto njiti, Doris Mollel na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya DTB, Betty Ruppia.

Wafanyakazi wa Benki ya DTB wakiwa na Muanzilishi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa pili kulia) kwa pamoja wakielekea kwenye wadi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki. Benki ya DTB walifika hospitalini kukabidhi msaada wa vifaa tiba na dawa za kuwasaidia watoto njiti ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto njiti duniani. DTB Bank imekuwa ikitoa misaada ya vifaa tiba kila mwaka kwa hospitali ya Amana na kwa mwaka huu wameamua kuwasaidia watoto njiti. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya DTB, Betty Ruppia.
Afisa Msaidizi wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi ya Mariam Gerion, akikabidhi sehemu ya zawadi kwa wakinamama waliojifungua watoto Nditi, katika Wadi ya Wazazi  Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
Wafanyakazi wa Benki ya DTB wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Doris Mollel, muda mfupi baada ya kumazika kwa zoezi la utoaji wa vifaa tiba na dawa, kwa hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya DTB, Betty Ruppia (kulia) akishirikiana na Rahma Amood kutoka Taasisi ya Doris Mollel pamoja na Afisa Usimamizi na Ubora wa hospitali ya Amana, Lucy Mbusi kupanda mti katika moja ya maeneo ya hospitali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...