Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

JESHI la Polisi  Makao Makuu  imeunda timu ya upelelezi ya kufatilia tukio la kushambuliwa kwa risasi  kwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Dodoma.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema ameunda  timu ya kufatilia tukio la  kushambulia kwa risasi kwa  mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu  jana mkoani Dodoma.

Amesema timu ya makao makuu ya Polisi inaenda kuongeza nguvu zaidi ili kuhakikisha kuwa watuhumiwa waliofanya kitendo hicho wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
IGP Sirro amesema kuwa waliomshambulia  Mwanasheria huyo na   Rais wa Chama Wanasheria Nchini (TLS) ni watu wasiofahamika  ambapo  hivi sasa anaendelea na matibabu.

Hata hivyo amesema kuwa Lissu alidai kuwa kuna watu wanafuatilia lakini hakuweza kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi hivyo akipona anatakiwa kupeleka taarifa hizo.

IGP Sirro amewataka wananchi kuacha kusambaza ujumbe na picha video za taarifa zisizo za ukweli kwenye mitandao ya jamii na matukio mbalimbali yanayotokea nchini kutokana na kuibua hofu kwa wananchi  pamoja na kuweza kuharibu upelelezi wa tukioa lilomtokea Lissu.

 Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi  kwa kutoa taarifa zitakazofanikisha kwa kukamatwa watuhumiwa wote waliohusika na tukio la Lissu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kutangaza kuwa Jeshi la Polisi  limeunda Timu maalum kwaajili ya kuchunguza na kufuatilia tukio la kushambuliwa kwa risasi hapo jana Mkoani Dodoma nyumbani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...