Jovina Bujulu-MAELEZO

Hivi karibuni, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea (TFRA) imeingiza nchini mbolea yenye uzito wa tani 55,000 kwa mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja bila kuwepo malipo ya ziada bandarini. 

Mfumo huo utasaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima wengi nchini.

Uingizwaji wa mbolea hiyo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2017/18, mjini Dodoma.

DKt. Tizeba alisema kuwa kuanzia msimu wa 2017/18  Serikali itaanza kuagiza mbolea kwa mfumo wa pamoja kwa kuanza kuagiza aina mbili za mbolea ambazo ni mbolea ya kupandia (DAP) na ya kukuzia (UREA), kwa kuwa ndizo  zinatumika sana nchini.

Alitaja sababu za kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja na kuongeza matumizi ya mbolea nchini kwa kuhakikisha kuwa wadau wote wanapata uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ushindani. 

Aidha, mfumo huo unawawezesha wafanyabiashara wadogo wanapata nafasi ya kuagiza mbolea na kuimarisha mtandao wa usambazaji hadi ngazi ya mkulima.

Vilevile utaratibu huo unawawezesha waagizaji kununua mbolea wakati bei ikiwa ndogo na TFRA  kufuatilia bei hiyo ili kuepuka mwanya wa waagizaji kuongeza bei zaidi ya ile iliyonunuliwa kwa bei ndogo

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...